Wakenya wenzangu,
Bona nchi yetu kawa janga la vita?
Nani katuambukiza shida hii kwani jambo geni ambalo hatujakuwa nalo hapo awali?
Wakaazi wa mitaa ya mabanda, unyama upi kawaingilia? Mbona mwauana pasipo sababu kamili na hata kama ipo mwavunja amri iliyoko katika maadiko matakatifu.
Wakenya, kwani uhusiano ambao tumekuwa nao hapo awali ulijengwa juu ya misingi ipi?
Nawaomba kwa hisani yangu, isiwe tumejenga uhusiano wetu juu ya misingi ya KIKABILA wala KISIASA.
Je, mie mkaazi wa mtaa wa Mabanda na uhusiano upi na wizi wa Kura iwapo ulikuwepo?
Nawauliza tena, mie mkaazi wa Mabanda na uhusiano upi na wizi wa Kura iwapo ulikuwepo?
Ni jambo la kutisha kuona jinsi wahadhiriwa walioishi katika mitaa ya mabanda wanavyo ishi katika uwanja wa Maonyesho wa Nairobi na pia katika uwanja ulioko Nakuru.
Jambo na kutisha ni Kuwa Atieno na Nyambura hutumia godoro moja kwa upendo.
Je, wakenya Wenzangu, mbona tusione haya na kukomesha uhasidi uliojidhihirisha?
Mie kikenya1@yahoo.com