TIGblogs TIG | TIGblogs GROUP TIGBLOGS LOGIN SIGNUP
TUSEME KISWAHILI
Tumearifiwa kwamba kunalo kundi la wanaTIG wanaoshughulikia tafsiri ya Kiswahili ya tovuti nzima. Tukiyangojea matokeo ya kazi yao kwa hamu, tumeamua kuunda ukumbi huu ili kuwapa wasemaji wa Kiswahili fursa kujadiliana, kuchangia fikra zao na kujieleza katika Kiswahili. Nia yetu ni kuwaunganisha wanaTIG ambao, vinginevyo, hawangeweza kuwasiliana. Tuyavunje mapingamizi yanayotuzuia, na baadaye tutaweza kuiendeleza na kuitukuza lugha yetu . Tunakaribisha maandishi ya aina yoyote: Visa vifupi, makala, madondo kutoka shajarani zenu nk. Ombi letu ni moja tu: tafadhali changieni katika Kiswahili.


Word on the street is that members of a TIG group are working on translating the website so that it will eventually be available in Kiswahili. In the meantime, this is a forum for all speakers of Kiswahili to exchange ideas and to express themselves in Kiswahili. We would like to build bridges connecting TIGers from different communities who may otherwise not be able to communicate with each other. Let us break down the barriers holding us back so that we may develop and promote our language. Stories, journal entries, poetry and any other writing are welcome. All that we ask is that you express yourself primarily in Kiswahili.



« previous 5


bumbuwazed   bumbuwazed Kahendi's TIGblog
Kahendi's profile

Lugha na Mikakati

Hapa Marekani, huwa sipati fursa nyingi kuongea Kiswahili. Mara kwa mara hutokea mtu anayekifahamu. Twaanza kuongea, lakini kila baada ya maongezi mafupi, twajikuta tukijitumbukiza katika kidimbwi cha Kimombo. Vilevile, nikijaribu kuandika Kiswahili, vikwazo vingi hutokea mbele yangu. Ni rahisi zaidi kwangu kutumia Kimombo.

Suala la lugha ni suala la kisiasa. Lakini zaidi ya hayo, ni suala la mawasiliano. Kila mtu hutamani kueleweka, na tena hutamani kumwelewa mwenziwe. Kila mwandishi anapoandika, huwa na makusudi ya kueneza ujumbe wake kokote kunakostahili. Hutekeleza lengo hili hususan kwa kuandika katika lugha itakayoelewa na watu wengi. Mara mengi, lugha hiyo siyo lugha ya mama, bali ni lugha ya kigeni, kama Kimombo au Kifaransa. Tatizo hufuata: kila anapoamua kutumia lugha hizi za kigeni, mwandishi hukosa nafasi ya kuendeleza lugha yake mwenyewe.

Ili kulitatua tatizo hili, hatuna budi kuyatafakari maswali kama haya yafuatayo kwa makini:
a) Mwandishi anawezaje kutekeleza wajibu wake wa kuhifadhi na kuendeleza lugha yake na mila yake?
b) Mwandishi anawezaje kutimiza lengo lake la kuandika maneno yatakayoelewa na kuthaminiwa na wanadamu wenye asili tofauti?

Maoni yenu?
================================================================================
(Rough Translation)

Language and Strategies

Here in the USA, I don't get many chances to speak Swahili. Once in a while, someone who understands the language comes along. We start to speak, but then after a short while, we fall into the trap of speaking English. Similarly, when I try to write in Swahili, I encounter many obstacles. I find it easier to write in English.

The language issue is a political issue, but more than that it is a communication issue. Everybody would like to be understood, and what’s more, would like to understand others. Every writer aims to spread his/ her message wherever is appropriate. He/ she achieves this most especially by writing in the language that the bulk of the target audience will understand. Often, that language is not his/ her mother tongue, but rather, a foreign language such as English or French. This gives rise to a problem: every time that the writer uses one of these foreign languages, he/ she loses a chance to develop his/ her own language.

To solve this problem, we have to reflect on the following questions:
a) How can the writer uphold his responsibility (that of preserving and developing his/ her language and traditions)?
b) How can the writer achieve his/ her goal and write words that will be understood and valued by people of different origins?

Your thoughts?

February 22, 2008 | 7:21 PM Comments  0 comments

Tags:


bumbuwazed   bumbuwazed Kahendi's TIGblog
Kahendi's profile

ALI MAZRUI: NGUGI KISWAHILI, KIKIKUYU
Related to country: Kenya



February 21, 2008 | 10:15 PM Comments  0 comments



bumbuwazed   bumbuwazed Kahendi's TIGblog
Kahendi's profile

Rais Bush nchini TZ
Related to country: Tanzania


http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/02/18/108663.html

Rais Bush Apagawisha

2008-02-18 19:49:24
Na Mwandishi Wetu, Jijini


Licha ya kutoka katika taifa lenye nguvu kubwa zaidi za kiuchumi duniani, Rais George W. Bush wa Marekani ameweza kujichanganya na Wabongo Jijini na kuwapagawisha maelfu ya waliofika kumpokea.

Bush, aliyewasili Jijini tangia Jumamosi jioni kwa ajili ya ziara ya kitaifa ya siku nne nchini, amefanya jambo hilo lisilokuwa la kawaida kwa marais wa taifa hilo walio madarakani na kuwashangaza hata maafisa wake wa Kikosi cha FBI.

Kwa ujumla, mambo yenyewe aliyoyafanya Rais Bush mara tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kuwapagawisha watu ni kama haya:

Ajitosa uswazi:
Awali ya yote, alipotua pale kwenye `terminal one`, Bush alitoa mpya wakati alipositisha ghafla zoezi lake la kupungia mkono watu waliokuja kumpokea na kisha kujichanganya nao kwa muda.

Ilianza kama masihara vile, Bush alichomoka ghafla toka kwenye kapeti kali jekundu alilokuwa akipitishwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Jakaya Kikwete.

Kisha kwa mastaajabu ya wengi, akamuendea mama mmoja aliyekuwa miongoni mwa watu tele waliokuwa wakimpungia na kukumbatiana naye. Jambo hilo liliamsha hisia kali za furaha na nderemo.

Jana, Bush akaendelea kujichanganya `uswazi`, kunako mitaa ya Buguruni na Ilala ambako, ingawa alikuwa akilindwa vikali, aliweza kutimiza ratiba yake ya kuzindua majengo mapya katika Hospitali ya Amana, yaliyofadhiliwa na Serikali yake.
Atema Kiswahili.

Wakati alipopewa fursa ya kuzungumza pale katika viwanja vya Ikulu, ambako yeye na mwenyeji wake walikutana na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, Rais Bush alibonga Kiswahili kwa namna isiyotarajiwa.

Alikamata mic, kisha akasalimia kwa kusema `Mambo viipiii!``
``Alinishangaza. Kamwe sikujua kama Rais Bush anaweza kutusalimia kwa Kiswahili,`` amesema Bw. John Jacob, mkazi wa Manzese Jijini.

Amwaga Mapesa
Pamoja na kuwapagawisha Wabongo kwa staili ya ujio wake na mivifaa ya kisasa ya kumlinda ikiwa ni pamoja na midege na migari myeusi ya bei mbaya, Rais Bush amewaletea neema Wabongo.

Yeye na mwenyeji wake, Rais Kikwete, wamesaini mkataba utakaoiwezesha Tanzania kupata msaada wa dola za Kimarekani Milioni 698 sawa na pesa za Kitanzania bilioni 800. Haijapata kutokea!

Pesa hizo zitatumika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kujengea miundombinu ya barabara.

Aidha, mke wa Rais Bush, Bi. Laura Bush, amemwaga msaada wa dola za Kimarekani Milioni 43 kwa mradi unaokwenda kwa jina la `Pamoja Inawezekana`, ulio chini ya Mama Salma Kikwete, kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima nchini.

SOURCE: Alasiri

February 18, 2008 | 9:05 PM Comments  0 comments



« previous 5


Owner
This Group TIGBlog is owned by: R Oburra.

Membership
Miguel
Christabell
Connie Wokuri
NKATHA
judy
Maxence M. Melo
David Diogène
Norma
Kahendi
Rahab
Terri
Terri-Ann Gilbert-Roberts
VICTOR RASUGU
Vitalis Wafula Wekesa

You must be logged in to join this group TIGblog.

Latest Posts
Utapiamlo (Malnutrition)
NI HUKUMU YA MUNGU AMA...
Siku iliyopita ...
Siku iliyopita ...
Ni vema kabisa ...

Monthly Archive
December 2007
January 2008
February 2008
March 2008
April 2008
May 2008
July 2008

Change Language



3847 views
Important Disclaimer