Ni vema kabisa kuelewa swala au mswaada wa mambo yanavyo endela nchini Kenya.Hivi tunavyozungumza, sheria mbili mwafaka za kuidhinisha ofisi ya Waziri mkuu na pia tume ya kuchunguza na kuhakikisha ukweli na haki zimeshatiwa sahihi na sasa zangojea tu kuandikishwa rasmi .
Twaona kwamba pia wanasiasa wameweza kuyaweka masilahi ya wakenya kwanza na kwa moyo wote kuunga mkono miswaada hii. Katika bunge, twaona ya kuwa Rais Kibaki alihudumu kikao hiki cha tatu kama Mbunge wa Othaya na wala si kama rais. Hii ni dhairi shairi kwamba pia yeye ameunga mikakati inayo endelea ya kuwezesha amani nchini Kenya. Chama cha ODM ambacho kilionekana kuweza kuanza kuwa na migogoro hivi karibuni , kupitia kwa msimamo ambao Kigogo wa Pentagon bwana Ruto aliokuwa ameuchukuwa, kimefikia maelewano ambayo yameleta utulivu. Bwana Ruto ametangaza hadharani kuwa anaunga mkono kuteuliwa kwa Bwana Musalia Mudavadi kama Naibu wa waziri mkuu. Bwana Ruto alitangaza haya akiwa katika eneo lake la bunge la allipohodhuria sherehe ya kuwatuza wanafunzi bora katika shule ya wanafunzi ya wasichna ya Eldoret.Musalia Mudavadi anayejulikana kwa umaarfufu kama ‘Double M’ , ni mbunge wa Sabatia katika mkoa wa Magharibi.
Twaomba kama wakenya na hasa wana TIG ya kuwa miswaada iliyoutiwa sahihi, itafuata kwa makini na kila anayehusika atatia for a na kufanya jukumu lake la kuhakikisha ya kuwa mambo yaliyojadiliwa yatatimizwa.